DAMU. SABABU ZA KUPUNGUA MWILINI na SIFA ZA MTU ANAYETAKIWA KUTOA DAMU





Habari za leo ndugu msomaji wa ELIMU YA AFYA?

Leo napenda kukuelimisha kuhusu vigezo vinavyotakiwa kwa mtu anayetaka kutoa damu. 

Damu ni kiungo muhimu sana mwilini kwa ajiri ya kusafirisha hewa safi ya Oxygen kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye moyo na pia kutoa hewa chafu ya Carbondioxide kutoka kwenye moyo na kuipeleka kwenye mapafu na hapo hewa hiyo chafu hutolewa nje.
Lakini pia ndani ya damu kuna kinga za mwili ambazo kwa jina la kitaalamu zinaitwa Immunoglobulins zinazotoa kinga zidi ya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Kwenye mwili wa mtu mzima kuna kiasi cha lita 5 hadi 6 za damu inayozunguka, hii inategemeana na uzito wake.

Naamini unajua kabisa kwamba damu ni uhai na mtu yeyote anapokuwa ana tatizo la upungufu wa damu huwa ana dalili za kuishiwa nguvu lakini pia kizunguzungu, kupoteza fahamu na hata kufa kabisa.
Mambo yanayosababisha mtu kupungukiwa damu ni;

  • Kuwa na malaria.
  • Ugonjwa wa minyoo hasa minyoo ya safura na kichocho.
  • Ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell Disease)
  • Kupata ajali
  • Kutokwa damu nyingi wakati wa upasuaji.
  • Upungufu wa damu kwenye ujauzito.

Vigezo vya kuzingatia kwa mtu anayetakiwa kutoa damu.

  • Awe ni mtu mwenye umri wa miaka kuanzia 18 hadi 60
  • Awe na wingi wa damu usiopungua 13.0g/dl
  • Asiwe mjamzito au ananyonyesha (Kwa mwanamke)
  • Asiwe mwenye tabia hatarishi kama kuwa na wapenzi wengi au utumiaji wa madawa ya kulevya.
  • Awe na anfya nzuri
  • Awe na uzito usiopungua kilogramu 50.
  • Asiwe na maambukizi ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya damu kama HIV, Ugonjwa wa ini (Hepatitis) na magonjwa ya zinaa.
  • Asiwe anatumia dozi ya aina yoyote
  • Mapigo yake ya moyo yawe kati ya 60 na 95
  • Aliyewahi kufanyiwa Upasuaji haruhusiwi kutoa damu. Anaweza kutoa damu kwa ruhusa maalumu kutoka kwa daktari.


Vipimo vinavyotakiwa kupimwa kabla ya mtu kuruhusiwa kutoa damu ni kama vile;

  • HIV Test
  • Wingi wa damu.
  • Uzito wa mtoa damu
  • Ugonjwa wa ini.
  • Magonjwa ya zinaa.
  • Mapigo ya moyo
  • Shinikizo la damu
  • Kisukari

Baada ya kupiwa vipimo hivyo, Mtoaji wa damu ataruhusiwa kama hivyo vipimo vitakuwa vizuri nikimaanisha kwamba havina matatizo.

Kwa Tanzania, kuna utaratibu wa utoaji damu ambapo kuna shirika la kiserikali linalohusika na maswala ya kutoa damu, shirika hilo linaitwa DAMU SALAMA. Huko wanakusanya damu kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama vile;

  • Mashuleni
  • Vyuoni
  • Makanisani
  • Misikitini
  • Kwenye mikusanyiko mbalimbali ya watu
  • Ndugu wa wagonjwa
  • Wachangiaji binafsi.

Baada ya kukusanya damu kutoka kwenye vyanzo hivyo hapo juu, DAMU SALAMA huchukua hiyo damu na kwenda kuipima ili iruhusiwe kutumika kwa ajiri ya mgonjwa. Vituo vya DAMU SALAMA hapa Tanzania vipo kama ifuatavyo;

  • Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam)
  • Kanda ya ziwa Mwanza Bugando)
  • Kanda ya magharibi (Tabora)
  • Kanda ya nyanda za juu kusini (Mbeya)
  • Kanda ya kaskazini (Moshi)

Pamoja na hivyo, kwenye hospitali za wilaya na mikoa damu huwa inakusanywa na kupelekwa kwenye ofisi za kanda husika za DAMU SALAMA kwa ajiri ya uchunguzi zaidi. Jinsi wanavyokusanya damu kwenye hizi Hospitali ni kwa njia ya kurudisha (Replacement) kutoka kwa ndugu wa wagonjwa walioongezewa damu tayari.
Nawaombeni sana tujilolee kutoa damu maana damu ni kidogo sana  na wahitaji mahospitalini ni wengi sana. Kwa hiyo naomba sana ndugu yangu wewe na mimi tuwe tayari kutoa damu ili tuwasaidie wanaoteseka kwa kukosa damu. Tukumbuke kuwa HAKUNA KUWANDA CHA KUTENGENEZA DAMU ILA NI MTU PEKEE ANAYEWEZA KUJITOLEA KWA HIARI YAKE. Nimesema hivyo nikimaanisha kwamba DAMU HAIUZWI. Kama mtu atataka kukuuzia damu fanya yafuatayo;

  • Kwanza kabisa mueleweshe kuwa damu haiuzwi, akikataa muulize kwamba hiyo damu anayoiuza ameitoa wapi?
  • Ikishindikana sana omba msaada kwa MGANGA MFAWIDHI WA HOSPITALI HUSIKA au kwa mkuu wa idara ambapo kuna mtu anayetaka kukuuzia damu (mf. Maabara, Chumba cha upasuaji, Wodini)
  • Au toa taarifa moja kwa moja polisi au PCCB 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

VIDONDA VYA TUMBO. (Dalili, Vipimo unavyotakiwa kupima na matibabu yake)

FAHAMU JINSI YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA AU ALIYEPATA MSHTUKO (SHOCK)

FAHAMU MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU YA VIPIMO MBALIMBALI YA MAABARA UKIWA HOSPITALI