FAHAMU JINSI YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA AU ALIYEPATA MSHTUKO (SHOCK)
Ni amtumaini yangu kuwa u mzima mpendwa msomaji wa makala hii.
Tumewapoteza ndugu zetu wengi sana au rafiki zetu au jamaa zetu wengi kwa sababu ya mshtuko(Shock) iliyosababisha kifo chao. Hii ni kwa sababu watu wengi hawajui jinsi ya kumsaidia mtu mwenye mshtuko kabla ya kumpeleka hospitali. Leo nakuletea makala inayokufundisha hatua zote za kufanya ili kumsaidia mtu mwenye mshtuko. Naomba uwe na mimi mpaka mwisho wa makala hii.
Kwenye somo langu lililopita nilikuelezea jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyepata ajali na leo naendelea kukufundisha kuhusu namna/jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyepata mshtuko.
Cha msingi kila mmoja anatakiwa kuwa na vifaa vyote au baadhi vya kufanyia huduma ya kwanza ambazo nilizitaja kwenye makala iliyopita ili tusaidiane wakati wowote.
Tuanze kwa kujua kuhusu mshtuko.
Damu huzunduka kwenye mwili wa binadamu kutoka kwenye moyo na kusambaa kwenye sehemu zote za mwili kwa kupitia mirija ya damu inayotumika kusafirishia hiyo damu, wakati huu damu inayozunguka mwilini huwa imebeba hewa ya oksijeni kwenye ogani (Organs) na misuli (Tissues) zote za mwili. hii hutokea kwenye hali ya kawaida ya moyo kufanya kazi.
MSHTUKO ni pale mfumo mzima wa kusafirisha damu mwilini unaposhindwa kufanya kazi vizuri. Hali hii hutokea mara nyingi baada yamtu kupata ajali, maumivu au ugonjwa wa ghafla (sudden illness) hasa hasa kama huu ugonjwa wa ghafla unaambatana namaumivu.
Sababu kubwa sana zinazoweza kusababisha mshtuko ni kuvuja damu kwa wingi inayozidi lita 1.2 kwa muda mfupi, upungufu wa maji mengi mwilini unaosababishwa na kuharisha, kutapika, utumbo kujisokota (intestinal obstruction) na kuungua moto.
Dalili za mtu aliyepata mshtuko;
Mtu mwenye mshtuko anaweza kukosa hewa kwenye akili, dalili zingine za mtu mwenye mshtuko ni;
- Mapigo ya moyo kwenda kwa kasi.
- Mgonjwa kuwa dhaifu.
- Mgonjwa anapauka mwili.
- Mwili kuwa wa baridi na ngozi kukakamaa.
- Kutokwa jasho.
- Anabadirika rangi Cyanosis) hasa kwenye midomo, vidole au kwenye masikio.
- Kizunguzungu.
- Kichefuchefu na hata kutapika.
- Anavuta pumzi kwa shida.
- Kiu.
- Kutokutulia lakini pia anakuwa mkali.
- Kupiga miayo sana.
- Kutokujitambua na mwisho moyo unashindwa kufanyakazi na mgonjwa anaweza kufa.
JINSI YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MTU MWENYE MSHTUKO.
- Kama unajua chanzo cha mshtuko mfano kuungua au kutokwa damu nyingi, ni bora zaidi ukatibu tatizo ili kupunguza uwezekano wa kuumiza ogani (Organs) za mwili na baada ya hapo uendelee kumpa hudumia kama nilivyokuandikia hapa chini.
- Mlaze mgonjwa chini sehemu ya wazi na yenye hewa safi. hakikisha ulipomlaza siyo pa baridi sana. weka miguu juu kidogo zaidi ya kichwa ili kusaidia damu kuzunguka hadi kwenye akili kichwani.
- mtie moyo mgonjwa mara kwa mara pindi anapoanza kuzinduka.
- Fungua na ulegeze sehemu zote za mwili wake ziliyofungwa na kukazwa kwa nguo zake kama kiunoni, shingoni mikononi n.k.
- Wakati unaendelea WAPIGIE SIMU WATU WENYE GARI LA KUBEBA WAGONJWA (ambulance)
- Mpime mgonjwa vipimo vya kuangalia mapigo ya moyo. (Nitatoa elimu jinsi ya kupima mapigo ya moyo kwenye masomo yajayo)
- Kama mgonjwa hajitambui kabisa. inabidi umfungue kwenye njia ya hewa na umuangalie kama anapumua vizuri. (utamtambua kwa kuangalia kama kifua kinapanda na kushuka hata kama ni kwa shida) Lakini kama hapumui vizuri tumia kiganja chako kusukuma kidogo kifua chake kuelekea ndani mara kwa mara huku ukiendelea kuangalia kama ameanza kupumua.
- Mshtuko (shock) ni ugonjwa unaotishia maisha ya binadamu kwani unatokea pale hewa safi ya oksijeni inapokosekana kwenye ogani mhimu za mwili kama vile akili, moyo na mapafu, kwa hiyo mgonjwa anahitaji huduma ya HARAKA SANA anapopatwa na mshtuko ili kuzuia uharibifu au kutokufanya kazi kwa ogani muhimu za mwili.
Kwa leo naomba niishie hapa lakini tukumbuke kuwa huduma ya kwanza inatolewa na mtu yeyote na si ya nesi na daktari tu. tuwajibike katika kuwasaidia ndugu zetu. Nakuomba uendelee kufuatilia makala hizi kwenye www.elimuafya.blogspot.com kwa masomo zaidi ya afya.
Emmanuel Shimbala (Lab. Tech)
Maelezo mazuri yanaeleweka ila maelezo zaidi ya namna gani ya kumlaza maana vijijini ikitokea wanamlaza mgonjwa wanavyo jua wao
JibuFuta