FAHAMU MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU YA VIPIMO MBALIMBALI YA MAABARA UKIWA HOSPITALI
Habari za leo ndugu msomaji wa makala hii?
Mimi ni mzima wa afya, Namshukuru sana Mungu kwa kunilinda na kuniongoza ili niweze kukufahamisha kuhusu muda unaotakiwa kuutumia wakati unasubiri majibu yako maabara.
Maabara kuna vipimo vya aina mbalimbali vinavyoweza kupimwa Maabara na lengo kubwa la mgonjwa kupimwa ni kupata matibabu sahihi.
Orodha ya vipimo niliyoandika hapa chini na muda wa kusubiria vinategemeana na Hospitali husika na idadi ya wahudumu (Wataalamu wa maabara) wanaohudumia, kwa hiyo ni vizuri kwa kila Hospitali kuweka wazi muda wa kusubiria majibu ya kila kipimo wanachopima (vyote)
Hapa ni baadhi ya vipimo ambavyo vinapimwa Maabara ni:
AINA YA KIPIMO
|
MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU
|
Fully
blood count (FBC) (Ni kipimo kinachotumika kupima magonjwa mengi yanayoweza kutokea kwenye damu kama kansa, n.k.)
|
Masaa manne 4 |
Haemoglobin (Wingi wa damu)
|
Dakika 20 hadi 30
|
Sick
ling test (Kupima ugonjwa wa Sickle Cell)
|
Masaa 24
|
CD4
|
Masaa 24
|
Blood
Slide (B/S) (Kipimo cha damu cha kuangalia malaria kwenye damu kwa kutumia darubini)
|
Saa moja.
|
Malaria
Rapid Diagnostic Test (mRDT) (Kipimo cha damu ili kuangalia malaria kwa kutumia kipimo maalumu cha haraka
|
Dakika 20 hadi 30 |
Urine
microscopy (Kipimo cha mkojo)
|
Saa moja. |
Stool
microscope (Kipimo cha haja kubwa)
|
Saa moja.
|
Blood
group and Rhesus factor (Kipimo cha kuangalia kundi la damu)
|
dakika 20 hadi 40
|
Cross
match (Kipimo cha kuangalia ulinganifu wa damu kati ya
|
Saa moja
|
VDRL/RPR (Kipimo cha damu ili kuangalia uwepo wa magonjwa ya zinaa)
|
masaa mawili.
|
Widal
(ext ended) test (Kipimo cha damu ili kuangalia uwepo wa Homa ya matumbo yaani Typhoid)
|
Masaa 24.
|
Cryptococcus
neo. test
|
masaa 2
|
Pregnancy
test (Kipimo cha kuangalia ujauzito kwenye mkojo)
|
Dakika 15 hadi 40.
|
HIV
test
|
Dakika 30.
|
Urine
for culture (Kuotesha wadudu walio kwenye mkojo)
|
Siku 3
|
Stool
for culture (Kuotesha wadudu kwenye Haja kubwa au kinyesi)
|
Siku 4
|
Urethral
and HVS for culture (Kuotesha wadudu kwenye majimaji ya kwenye uti wa mgongo)
|
Siku 3
|
CSF
for bacteriological test (Kipimo cha majimaji ya kwenye uti wa mgongo ili kuangalia uwepo wa Bakteria)
|
Masaa 4
hadi 72
|
Gram
stain (Kipimo cha kuangalia kama kuna bakteria kwenye aina yoyote ya kipimo)
|
Saa moja. |
Sputum for AFB (Makohozi)
|
Masaa 24hrs hadi 48.
|
ASAT (Kipimo cha damu ili kuangalia kama ini linafanya kazi vizuri)
|
Masaa 6 hadi 24
|
ALAT (Kipimo cha damu ili kuangalia kama ini linafanya kazi vizuri)
|
Masaa 6 hadi 24
|
Criatinine (Kipimo cha damu ili kuangalia kama figo zinafanya kazi vizuri)
|
Masaa 6 hadi 24
|
Glucose (Kipimo cha sukari kwenye damu)
|
Masaa 6 hadi 24
|
CSF
Glucose (Majimaji ya kwenye uti wa mgongo ili kutambua kama kuna sukari ndani yake)
|
Saa moja hadi masaa 6.
|
Urine
for urinalysis (Kipimo cha mkojo ili kuangalia vipimo mbalimbali kama protein, Sukari, Albumin n. k.)
|
Saa moja.
|
Maoni
Chapisha Maoni