VIDONDA VYA TUMBO. (Dalili, Vipimo unavyotakiwa kupima na matibabu yake)

Karibu tena kwa mara nyingine msomaji wa makala hii ya ELIMU YA AFYA ambapo leo tutazungumzia kuhusu madonda ya tumbo.

Maana yake.
Madonda ya tumbo ni matokeo baada ya kukosekana kwa uwiano kati ya enzaimu (Enzymes) zinazosaidia kumeng'enya chakula kwente tumbo na kwenye utumbo mwembamba.Asilimia kubwa ya madonda ya tumbo husababishwa na bakteria wanaoitwa Hericobacter pylori.

Vitu vinavyoweza kusababisha mtu kupata madonda ya tumbo ni;
  • Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza maumivu kama Asprin, Bruphen n.k.
  • Kutokula au kuchelewa kula. Hii inasababisha kutolewa kwa tindikali nyingi kwenye nyongo na kuenea tumboni na baadae kusababisha nyongo kuzalisha tindikali nyingi zaidi mwilini ambayo itakuwa kama sumu mwilini na kuushambulia utumbo.
  • Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kwa muda mrefu. Dawa kama aspirin, ibuprofen, na zingine za kutuliza maumivu zinaweza kusababisha madonda ya tumbo. Kwa hiyo fuata ushauri wa Daktari kabla hujaanza kumeza dawa hizi.
  • Uvutaji wa sigara.
  • Ulevi wa pombe wa kupindukia.
Dalili za Madonda ya tumbo.
Kwa dalili za mwanzoni mgonjwa atajisikia kama ifuatavyo;
  • Kupata kiungulia.
  • Tumbo kuuma hasa tumbo la katikati au juu. hii inaweza kutokea kabla ya kula chakula au usiku.
  •  Kupata kichefuchefu na hata wakati mwingine kutapika.
  • Kucheua mara kwa mara.
Kama ugonjwa utaendelea kukua zaidi unaweza kupata dalili zifuatazo;
  • Kupata choo yenye rangi nyeusi (kwa sababu ya kutoka damu kwenye utumbo)
  • Kutapika damu.
  • Kupungua uzito na
  • Maumivu makali tumboni.
Ukiona dalili hizi ni vizuri ukawahi mapema Hospitali kwa ajiri ya kupata vipimo na kupata matibabu zaidi.

Ukifika hospitali muelezee daktari dalili zote jinsi unavyojisikia. Kama daktari atahisi kuwa una ugonjwa wa madonda ya tumbo atakuandikia kwenda kupima vipimo kama nilivyoeleza hapa chini;

VIPIMO UNAVYOTAKIWA KUPIMA ILI KUTAMBUA UWEPO WA MADONDA YA TUMBO:
Daktari atakuandikia ukapime vipimo vifuatavyo;
  • Kipimo cha damu (H-Pylori Test). Hiki ni kipimo kinachoweza kutambua uwepo wa bakteria wanaoitwa Hericobacter pylori ambao ndio chanzo kikubwa cha madonda ya tumbo siku hizi. Hapa mtaalamu wa maabara atakuchukua damu kidogo kwenye kidole au kwenye mshipa ili kukufanyia kipimo hiki.
  •  Kipimo cha haja kubwa. (Stool for Culture) hiki kipimo hufanyika kwa kuotesha wadudu waliopo kwenye haja kubwa (Kinyesi) kwa siku kadhaa na kama kuna H-Pylori ndani yake ataota. Mtaalamu wa maabara atafanya kipimo kingine juu yake ili kujua dawa ya kuweza kumuua huyu mdudu.
  • barium swallow au upper GI series (gastrointestinal series).  Hapa mgonjwa atapewa kinywaji chenye kiasi kidogo cha mionzi. Daktari au mtaalamu atachukua picha nyingi za X-Ray ili kuona jinsi kile kinywaji ulichokunywa kinavyopita kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Hiki kipimo kinasaidia kugundua matatizo mengine pia ya tumboni.
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Matibabu ya vidonda vya tumbo hutegemeana na chanzo chake na ukubwa wa ugonjwa na dalili zake. Mfano;
  • Kama daktari wako atagundua kuwa madonda hayo yamesababishwa na matumizi ya dawa za kupunguza maumivu, Atakuandikia utumie dawa ya kuzuia nguvu ya dawa ulizotumia, dawa hizo ziko kwenye makundi ya dawa zinazoitwa histamine receptor blockers (H2 blockers) au kundi lingine la dawa linaitwa proton pump inhibitors (PPIs) ambazo hutumika kupunguza kiasi cha tindikali tumboni.
  • Kama vidonda vimesababishwa na bakteria wanaoitwa H-pylori, daktari atakupa aina fulani ya dawa za kuua hawa bakteria (Antibiotics) hizi dawa husaidia kuweka sawa sehemu ya utumbo iliyoharibika na kupunguza maumivu ya tumbo.
  • Kama dawa  hazitafanya kazi vizuri basi daktari wako anaweza kuamua kukufanyia upasuaji ili kukutibu tatizo lako.
Mwisho kabisa nakushauri sana ndugu na rafiki yangu kuwa usikae muda mrefu bila kupima afya yako. PIMA MARA KWA MARA ili kupunguza gharama za kutibu matatizo yakiwa makubwa.

Maoni

  1. Ahsante je ni umri gani ambao MTU? anaweza kuugua madonda tumbo

    JibuFuta
  2. Mm Nina vidonda vya tumbo hangamito zake ,tumbo kuwaka moto,mgongo chini ya mabega,kichwa kuuma ,kichefu chefu ,kutapika,je kutokana na dalili zangu hizo je vidonda tumbo hivyo vimefikia steji gani?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAHAMU JINSI YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA AU ALIYEPATA MSHTUKO (SHOCK)

FAHAMU MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU YA VIPIMO MBALIMBALI YA MAABARA UKIWA HOSPITALI