HUDUMA YA KWANZA KWA MGONJWA ANAYETOKWA DAMU PUANI

Ni matumaini yangu kuwa u mzima mpenzdwa msomaji wa ELIMU YA AFYA.

Leo napenda kuongea na wewe kuhusu jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu anayetokwa damu puani.

Tatizo la kutokwa na damu puani husababishwa na kupasuka kwa mishipa midogomidogo inayosambaza damu puani. Tatizo hili hutokea kwenye tundu moja ama yote ya pua na linaweza kusababisha hata kifo kama halitapatiwa ufumbuzi kwa muda muafaka.

Nini sababu za kutokwa na damu puani?
Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha mtu kutokwa na damu puani na miongoni mwa hizo sababu ni;
  • Kupasuka kwa mirija ya damu inayopeleka damu kwenye maeneo ya pua.
  • Shinikizo la damu kuongezeka (High blood pressure)
  • Kupiga chafya (sneezing)
  • Kupenga kwa nguvu.
Jinsi ya kutoa huduma kwa mtu anayetokwa damu puani.
  • Mruhusu mginjwa akae. (Usimlaze chali maana damu inaweza kurudi na kuziba mirija ya hewa na mgonjwa akashindwa kupumua)
  • Hakikisha milango ya hewa (Mdomo) iko wazi ili mgonjwa aendelee kupata hewa safi ya Oksijeni.
  • Mkalishe akiwa ameinama kidogo kuelekea mbele.
  • Binya kidogo matundu ya pua yake kwa muda kidogo. (Mgonjwa mwenyewe anaweza kufanya hivi pia kama hajazidiwa sana)
  • Mwambie avute hewa kupitia mdomo na siyo pua maana utakuwa umeiziba.
  • Baada ya muda kidogo achia halafu uangalie kama damu imeacha kutoka.
  • Endelea kwa utaratibu huu (wa kubinya pua na kuachia baada ya muda) kama mara nyingi.
  • Kama damu haijaacha kutoka kwa muda wa dakika 30, basi MWAHISHE MGONJWA WAKO HOSPITALI kwa matibabu zaidi

ZINGATIA
Kama mtu anatokwa damu puani, lengo lako kubwa la kumsaidia ni kuhakikisha unaondoa au unapunguza tatizo la damu kuendelea kutoka kwa mtu huyu.
Wakati unaendelea kumsaidia mgonjwa, mwambie azingatie haya;
  1. Asiongee.
  2. Ajizuie kukohoa.
  3. Asiteme mate.
Kumzuia mgonjwa kufanya niliyokueleza hapo juu ni ili kuzuia kuharibu mabongemabonge ya damu ambayo yanaweza kuwa yamejitengeneza puani na kusababisha damu ziendelee kutoka

Kwa leo naomba kuishia hapo.

Endelea kuwa nasi kwenye makala zijazo.

Maoni

  1. Nashukuru kupata msaada huu kwani nitanufaika nayo

    JibuFuta
  2. Nataka kutoa ushuhuda kuhusu jinsi nilivyopona kutokana na Virusi vya Herpes. Miezi michache iliyopita nilikuwa na dalili kadhaa. Nilienda kumuona daktari na vipimo vingi vya damu vilifanywa kwangu, baadaye niliambiwa nilikuwa na Herpes. Daktari wangu aliniambia kwamba hakuna tiba ya Herpes. Nilijisikia vibaya, niliingia mtandaoni nikitafuta tiba inayowezekana ya Virusi vya Herpes, niliona chapisho la Dkt. Dawn, daktari wa mitishamba anayewasaidia watu kupona kutokana na Herpes. Saratani. VVU na mengineyo. Niliwasiliana naye na kumwambia jinsi ninavyohisi. Alisema dawa yake ya mitishamba inaweza kuniponya. Alinitumia dawa kupitia huduma ya utoaji wa UPS na nilipokea dawa siku 6 baada ya kuituma, nilichukua dawa kama alivyoniagiza. Kabla sijakamilisha dawa dalili zilisimama. Nilienda kwa daktari na kufanya kipimo kingine cha damu, cha kushangaza nilikuwa hasi. Sijapata dalili tena. Dkt. Dawn ni mzuri na unaweza
    kuwasiliana kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Gmail ( dawnacuna314@gmail.com )

    Ikiwa unahitaji dawa za mitishamba kutibu magonjwa yoyote sugu au ya zinaa kama.
    HERPES.
    SARATANI.
    VVU/UKIMWI na zaidi

    JibuFuta
  3. Jina langu ni Vanessa Delarue.

    Ninatoa ushuhuda huu kuthibitisha uwezo wa mzee wa ajabu.

    Nakuhakikishia kwamba niliwasiliana na marabouts kadhaa ambao walikuwa wadanganyifu, waongo, walaghai—sijui niwaite nini tena. Lakini baada ya kutafuta sana, nilikutana na mzee huyu ambaye alinirudishia furaha yangu kweli, furaha ambayo nimekuwa nikitafuta kwa miaka mingi. Yeye ni mzuri sana. Nilikuwa nikiteseka kutokana na kutengana na mume wangu; aliniacha mwaka mmoja na mwezi mmoja uliopita. Hata nilipoteza kazi yangu. Baba yangu alikuwa mgonjwa sana, lakini ndani ya siku tatu, nakuhakikishia, miujiza imetokea maishani mwangu kutokana na mzee huyu. Leo, ninaishi vizuri na mume wangu, baba yangu amepona, niliitwa kurudi kazini, na hata nilikataa, lakini sasa niko katika idara tofauti ambayo ni bora kuliko nyingine. Sijui jinsi ya kumshukuru mzee huyu. Alinifanyia kazi bila kunitoza euro moja. Nilihisi kuridhika kwanza kabla ya kumzawadia. Yeye ni mzuri sana.
    Kwa hivyo, ikiwa una tatizo lolote, ikiwa una wasiwasi wowote, usijali tena. Wasiliana na mzee huyu moja kwa moja. Hapa kuna
    Anwani yake ya WhatsApp: +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAHAMU JINSI YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA AU ALIYEPATA MSHTUKO (SHOCK)

VIDONDA VYA TUMBO. (Dalili, Vipimo unavyotakiwa kupima na matibabu yake)

FAHAMU MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU YA VIPIMO MBALIMBALI YA MAABARA UKIWA HOSPITALI