FAHAMU MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU YA VIPIMO MBALIMBALI YA MAABARA UKIWA HOSPITALI
Habari za leo ndugu msomaji wa makala hii? Mimi ni mzima wa afya, Namshukuru sana Mungu kwa kunilinda na kuniongoza ili niweze kukufahamisha kuhusu muda unaotakiwa kuutumia wakati unasubiri majibu yako maabara. Maabara kuna vipimo vya aina mbalimbali vinavyoweza kupimwa Maabara na lengo kubwa la mgonjwa kupimwa ni kupata matibabu sahihi. Orodha ya vipimo niliyoandika hapa chini na muda wa kusubiria vinategemeana na Hospitali husika na idadi ya wahudumu (Wataalamu wa maabara) wanaohudumia, kwa hiyo ni vizuri kwa kila Hospitali kuweka wazi muda wa kusubiria majibu ya kila kipimo wanachopima (vyote) Hapa ni baadhi ya vipimo ambavyo vinapimwa Maabara ni: AINA YA KIPIMO MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU Fully blood count ( FBC ) (Ni kipimo kinachotumika kupima magonjwa mengi yanayoweza kutokea kwenye damu kama kansa, n.k.) Masaa manne 4 Haemoglobin (Wingi wa damu) Dakika 20 hadi 30 Sick ling test (Kupima ugonjwa wa Sickle Cell)...