Sehemu ya pili: MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANDAA SAMPULI KWA AJIRI YA UCHUNGUZI ZAIDI MAABARA
Habari za leo tena mpenzi msomaji wa makala hii? Ni matumaini yangu kuwa hujambo kabisa.
Karibu sana kwenye mwendelezo ya maada yetu ambayo ilikuwa inazungumzia MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANDAA SAMPULI KWA AJIRI YA UCHUNGUZI MAABARA ambapo nilikueleza kuhusu sampuli anazoweza kuandaa mgonjwa mwenyewe.
Leo nitakueleza kuhusu sampuli zinazochukuliwa na MTAALAMU.
Kabla sijaanza kukuelimisha hilo napenda ujue kuhusu uhusiano kati ya mgonjwa na mtoa huduma.
Hawa watu wawili wanategemeana sana ili mgonjwa apate majibu sahihi na mtoa huduma ajisikie vizuri baada ya kutoa huduma inayotakiwa kwa mgonjwa. Mtaalamu wa afya huwa anajisikia vizuri sana anapomhudumia mgonjwa ambaye ataonesha ushirikiano katika huduma yote atakayoipata kwake, vilevile pia mgonjwa atajisikia vizuri sana anapohudumiwa na mtaalamu anayesikiliza shida zake.
Kwa maana hiyo, kumbe wote wawili wanategemeana.
Kama mgonjwa ama mtoa huduma (mmoja kati yao) hatatoa ushirikiano, basi huduma yote kwa ujumla inaweza kuwa mbaya. Mfano; kama mgonjwa atafika Hospitali nakumkuta mtaalamu wa afya ambaye ni mkali, mwenye majibu ya kukatisha tamaa, anaweza kughairi kuhudumiwa kwake na kwenda sehemu nyingine. Lakini pia, mgonjwa anatakiwa kutimiza yote atakayohitajika kutimiza akiwa Hospitali kama vile, Kueleza matatizo yake yote kwa Daktari, Kutoa ushirikiano pale ambapo daktari ama mtoa huduma atahitaji kumfanyia uchunguzi zaidi.
Kwa hiyo; "HUDUMA BORA KWA MGONJWA INATOKANA NA USHIRIKIANO KATI YA MGONJWA NA MTOA HUDUMA"
Nimesisitiza hili kwa sababu vipimo ambavyo nakueleza leo vinahitaji zaidi ushirikiano kati ya mgonjwa na Daktari ama mtoa huduma.
Nakuomba tuwe pamoja kwenye mwendelezo wa maada hii..
Kwenye makala iliyopita tuliongelea kuhusu sampuli zinazoandaliwa na mgonjwa mwenyewe. Leo nitakueleza kuhusu sampuli zinazochukuliwa na mtaalamu wa maabara.
SAMPULI ZINAZOCHUKULIWA/KUANDALIWA NA MTAALAMU ni sampuli ambazo zinahitaji utaalamu wa hali ya juu sana ili kuvichukua kwa mgonjwa. Vipimo hivi hufanyiwa uchunguzi na mtaalamu aliyesomea fani ya maabara ili kumpatia mgonjwa huduma/matibabu sahihi.
Sampuli zinazochukuliwa namtaalamu ni kama vile;
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKULIWA KIPIMO.
Kuna mambo mengi sana ambayo unatakiwa kuzingatia kama unachukuliwa kipimo, baadhi ya hayo mambo ni;
Emmanuel Shimbala (Lab. Tech.)

- Damu.
- majimaji ya kwenye uti wa mgongo (Cerebral Spinal fluids)
- Vipande vya nyama kutoka sehemu yoyote ya mwili.
- Usaha
- Majimaji kutoka sehemu yoyote ya mwili (any body fluid sample)
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKULIWA KIPIMO.
Kuna mambo mengi sana ambayo unatakiwa kuzingatia kama unachukuliwa kipimo, baadhi ya hayo mambo ni;
- Kama kipimo kinachotakiwa ni cha damu kwa mtoto ama mkubwa, hakikisha mikono yako au ya mtoto ni safi. Fuata maelekezo kutoka kwa mtaalamu ili uhudumiwe vizuri zaidi.
- Kwa vipimo vingine vilivyobaki, fuata maelekezo kutoka kwa mtaalam.
Emmanuel Shimbala (Lab. Tech.)
Maoni
Chapisha Maoni