Sehemu ya pili: MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANDAA SAMPULI KWA AJIRI YA UCHUNGUZI ZAIDI MAABARA
Habari za leo tena mpenzi msomaji wa makala hii? Ni matumaini yangu kuwa hujambo kabisa. Karibu sana kwenye mwendelezo ya maada yetu ambayo ilikuwa inazungumzia MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANDAA SAMPULI KWA AJIRI YA UCHUNGUZI MAABARA ambapo nilikueleza kuhusu sampuli anazoweza kuandaa mgonjwa mwenyewe. Leo nitakueleza kuhusu sampuli zinazochukuliwa na MTAALAMU. Kabla sijaanza kukuelimisha hilo napenda ujue kuhusu uhusiano kati ya mgonjwa na mtoa huduma. Hawa watu wawili wanategemeana sana ili mgonjwa apate majibu sahihi na mtoa huduma ajisikie vizuri baada ya kutoa huduma inayotakiwa kwa mgonjwa. Mtaalamu wa afya huwa anajisikia vizuri sana anapomhudumia mgonjwa ambaye ataonesha ushirikiano katika huduma yote atakayoipata kwake, vilevile pia mgonjwa atajisikia vizuri sana anapohudumiwa na mtaalamu anayesikiliza shida zake. Kwa maana hiyo, kumbe wote wawili wanategemeana. Kama mgonjwa ama mtoa huduma (mmoja kati yao) hatatoa ushirikiano, basi huduma yote kwa ujumla inaweza ...