Machapisho

DAMU. SABABU ZA KUPUNGUA MWILINI na SIFA ZA MTU ANAYETAKIWA KUTOA DAMU

Picha
Habari za leo ndugu msomaji wa ELIMU YA AFYA? Leo napenda kukuelimisha kuhusu vigezo vinavyotakiwa kwa mtu anayetaka kutoa damu.  Damu ni kiungo muhimu sana mwilini kwa ajiri ya kusafirisha hewa safi ya Oxygen kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye moyo na pia kutoa hewa chafu ya Carbondioxide kutoka kwenye moyo na kuipeleka kwenye mapafu na hapo hewa hiyo chafu hutolewa nje. Lakini pia ndani ya damu kuna kinga za mwili ambazo kwa jina la kitaalamu zinaitwa Immunoglobulins zinazotoa kinga zidi ya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu. Kwenye mwili wa mtu mzima kuna kiasi cha lita 5 hadi 6 za damu inayozunguka, hii inategemeana na uzito wake. Naamini unajua kabisa kwamba damu ni uhai na mtu yeyote anapokuwa ana tatizo la upungufu wa damu huwa ana dalili za kuishiwa nguvu lakini pia kizunguzungu, kupoteza fahamu na hata kufa kabisa. Mambo yanayosababisha mtu kupungukiwa damu ni; Kuwa na malaria. Ugonjwa wa minyoo hasa minyoo ya safura na kichocho. Ug...

KUIMBA KUNA FAIDA KIAFYA

Picha
Habari za leo ndugu msomaji wa ELIMU AFYA? Leo nitaongelea kuhusu faida za kuimba ambazo zinamsaidia mtu kiafya. Kwanza kabisa naomba nikueleze maana ya kuimba. KUIMBA ni kutoa sauti yenye ulinganifu, sauti hiyo inatakiwa kufuata mapigo ya ki muziki na ni zaidi ya kughani. Zamani mababu zetu walikuwa wanaimba kwenye kazi mbalimbali ili kurahisisha kazi yenyewe iliyokuwa ikifanyika, mpaka sasa watu wengi huimba ili kuburudisha, kufundisha, kukosoa au kuelimisha kikundi fulani cha watu. Kuimba ni faida kwa mwimbaji kwani kuna faida nyingi saana ambazo mwimbaji anazipata kama vile kuburudika, kuburudisha, kuinjilisha, kuhamasisha, kufariji, kufurahisha n.k Leo nitakueleza faida za kuimba ambazo zinamsaidia mwimbaji kiafya, Faida zenyewe ni: Kuimba ni mazoezi. Unapoimba unafanya mazoezi ambayo pia ni kinga kwa magonjwa mbalimbali yanayoweza kumuathiri mtu ambaye hafanyi mazoezi. Mazoezi ambayo nayasemea hapa ni Kupanua kiwambo (diaphragm), mwanakwaya anatumia nguvu nyin...

FAHAMU MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU YA VIPIMO MBALIMBALI YA MAABARA UKIWA HOSPITALI

Picha
Habari za leo ndugu msomaji wa makala hii? Mimi ni mzima wa afya, Namshukuru sana Mungu kwa kunilinda na kuniongoza ili niweze kukufahamisha kuhusu muda unaotakiwa kuutumia wakati unasubiri majibu yako maabara. Maabara kuna vipimo vya aina mbalimbali vinavyoweza kupimwa Maabara na lengo kubwa la mgonjwa kupimwa ni kupata matibabu sahihi. Orodha ya vipimo niliyoandika hapa chini na muda wa kusubiria vinategemeana na Hospitali husika na idadi ya wahudumu (Wataalamu wa maabara) wanaohudumia, kwa hiyo ni vizuri kwa kila Hospitali kuweka wazi muda wa kusubiria majibu ya kila kipimo wanachopima (vyote)   Hapa ni baadhi ya vipimo ambavyo vinapimwa Maabara ni: AINA YA KIPIMO MUDA WA KUSUBIRIA MAJIBU Fully blood count ( FBC ) (Ni kipimo kinachotumika kupima magonjwa mengi yanayoweza kutokea kwenye damu kama kansa, n.k.) Masaa manne 4 Haemoglobin (Wingi wa damu) Dakika 20 hadi 30 Sick ling test (Kupima ugonjwa wa Sickle Cell)...