Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017

DAMU. SABABU ZA KUPUNGUA MWILINI na SIFA ZA MTU ANAYETAKIWA KUTOA DAMU

Picha
Habari za leo ndugu msomaji wa ELIMU YA AFYA? Leo napenda kukuelimisha kuhusu vigezo vinavyotakiwa kwa mtu anayetaka kutoa damu.  Damu ni kiungo muhimu sana mwilini kwa ajiri ya kusafirisha hewa safi ya Oxygen kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye moyo na pia kutoa hewa chafu ya Carbondioxide kutoka kwenye moyo na kuipeleka kwenye mapafu na hapo hewa hiyo chafu hutolewa nje. Lakini pia ndani ya damu kuna kinga za mwili ambazo kwa jina la kitaalamu zinaitwa Immunoglobulins zinazotoa kinga zidi ya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu. Kwenye mwili wa mtu mzima kuna kiasi cha lita 5 hadi 6 za damu inayozunguka, hii inategemeana na uzito wake. Naamini unajua kabisa kwamba damu ni uhai na mtu yeyote anapokuwa ana tatizo la upungufu wa damu huwa ana dalili za kuishiwa nguvu lakini pia kizunguzungu, kupoteza fahamu na hata kufa kabisa. Mambo yanayosababisha mtu kupungukiwa damu ni; Kuwa na malaria. Ugonjwa wa minyoo hasa minyoo ya safura na kichocho. Ug...