KUIMBA KUNA FAIDA KIAFYA
Habari za leo ndugu msomaji wa ELIMU AFYA? Leo nitaongelea kuhusu faida za kuimba ambazo zinamsaidia mtu kiafya. Kwanza kabisa naomba nikueleze maana ya kuimba. KUIMBA ni kutoa sauti yenye ulinganifu, sauti hiyo inatakiwa kufuata mapigo ya ki muziki na ni zaidi ya kughani. Zamani mababu zetu walikuwa wanaimba kwenye kazi mbalimbali ili kurahisisha kazi yenyewe iliyokuwa ikifanyika, mpaka sasa watu wengi huimba ili kuburudisha, kufundisha, kukosoa au kuelimisha kikundi fulani cha watu. Kuimba ni faida kwa mwimbaji kwani kuna faida nyingi saana ambazo mwimbaji anazipata kama vile kuburudika, kuburudisha, kuinjilisha, kuhamasisha, kufariji, kufurahisha n.k Leo nitakueleza faida za kuimba ambazo zinamsaidia mwimbaji kiafya, Faida zenyewe ni: Kuimba ni mazoezi. Unapoimba unafanya mazoezi ambayo pia ni kinga kwa magonjwa mbalimbali yanayoweza kumuathiri mtu ambaye hafanyi mazoezi. Mazoezi ambayo nayasemea hapa ni Kupanua kiwambo (diaphragm), mwanakwaya anatumia nguvu nyin...